Thursday, May 2, 2013

Watanzaia wautingisha Mji wa Koloni Ujerumani!

Chereko ! Chereko za Sherehe za miaka 49 ya muungano wa Tanzania !

Siku ya Jumamosi 27.04.2013 Watanzania Wanaoishi Ujerumani , chini ya mwamvuli wa umoja wao (UTU) Waliuhakikishia ulimwengu kuwa neno "MUUNGANO" lina maana
kamili kwa maisha ya  mtanzania na binadamu wengine.

Sherehe hizo zilizowakusanya watanzania na marafiki wa Tazania kutoka kila kona  ya ujerumani, ziliutingisha mji wa koloni katika Usiku usio kwisha wa kusherehekea miaka 49 ya muungano wa Tanzania.

Mhe.Ali Siwa naibu balozi wa Tanzania nchini Ujerumani alikua mstari wa mbele akiwaongoza watanzania katika Muungano Day,
Wasanii mbali mbali walitumbuiza jukwaani na kuipeperusha vilivyo bendera ya Tazania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania ujerumani Mh.Mfundo na kamati yake wameahidi
kufanya mambo makubwa na kuitangaza  Tanzania kwa hali na mali chini  ya  Umoja wa watanzania Ujerumani(UTU)

No comments:

Post a Comment