Kauli ya waziri wa Ardhi Bunge inawapa mashaka wakazi wa Kigamboni,
Mpango wa siri ya kuwafukuza wenyeji wa Dar na kuwaweka wageni ndio
Agenda ya Wizara ya Ardhi,
Watanzania sasa tuna miaka 51 ya Uhuru,lakini tupoangalia tutajikuta
tunaingia katika migogoro ya Ardhi na uvunjivu wa amani
utakaosababishwa
na Ardhi.
Ni mda mchache tu huko bungeni Dodoma waziri wa ardhi Mhe.Bi Anna
Tibaijuka ameliezea bunge kuwa nyumba takribani elfu 30 zitajengwa na
makampuni ya Dubai na Wachina, na wakazi wa Kigamboni watakuwa na hisa !
Kauli hiyo ya waziri Anna Tibaijuka inawatia wasi wasi wananchi na kujiuliza
maswali mengi kama vile kuwa na hisa katika biashara hipi? nani mmiliki wa
Ardhi? mbona wananchi wa Kigamboni hawajapewa taarifa yoyote!
hakuna kikako chochote kile kilicho washirikisha wananchi na kujua
hatima yao ! mbuge wa Kigamboni Mhe.Ndugulile naye kashangazwa na
kauli ya Waziri.
TATIZO LA KUWAMILIKISHA ARDHI WAWEKEZAJI LITALETA UTATA,
Wenyeji wa asili ya mikoa ya Dar-es-salaam na Pwani, wamejawa na unyonge
na kujiona wapo katika kilio cha kusaga meno kwa kuondolewa katika sehemu
zao za asili na kutojua wapi watapelekwa,
Tabia za baadhi ya wajanja kumiliki mashamba makubwa nalo limekuwa ugonjwa
ulijitokeza katika kumiliki Ardhi.
UVUNJWAJI WA SHERIA ZA ARDHI
Migogoro mingi ya Ardhi inatokana na uvunjwaji wa sheria zilizopo
na wizara inahusika kwa namna moja au ingine katika kuvunja sheria hizo,
Kuna
Ardhi zinazomilikiwa kimila,pia na manispaa, lakini Wizara ya ardhi
imekuwa ikiwanyang'anya wazawa na kuwapa wawekezaji wa kigeni ardhi
hizo bila ya kuwashirikisha wahusika,wananchi,serikali za mitaa na manispaa.
Ni juzi tu wakazi wa eneo la Tuangoma, njia panda ya Amani beach huko
Kimbiji walijikuta wanabobolewa majumba na kulazimishwa kulipwa
fidia la Sh.700,000 kwa heka ! na muwekezaji wa Kichina ndio kaanza
kazi? Wanajeshi nao wanajaribu kuwatishia maisha wanye mashamba
ili wapate mashamba ya bure.
Serikali ilitupia jicho tatizo la Ardhi tusije tukawa watumwa katika nchi yetu.