FELIS MWAMBALO MUBIBYA KUINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA KUANDAA NA KUSAMBAZA MZIKI NCHINI MAREKANI



Mumbaji mwenye vipaji mbalimbali Felis Mwambalo Mubibya ameingia mkataba  na kiwanda au kampuni ya kuandaa, kutangaza na kusambaza mziki iitwayo Tate Music Group (TMG) ipatikanayo Mustang, Oklahoma, katika Jamhuri ya Muungano wa Kimarekani.

TMG waliamua kuingia mkataba huu na muimbaji Felis, baada ya kuupenda mziki toka kwenye albamu yake mpya iitwayo Jipe Moyo/ Take Heart. Kazi hii ilirekodiwa na Fnouk Music Studios ya Arusha, Tnzania, East Africa na kukamilishwa au kufanyiwa mastering na Audio Recording Studio (ARS) ya Homewood, Illinois, USA.

Album hii ambayo imekaribia steji yakuwa hewani na madukani katika kampuni hiyo inayo m'miliki muimbaji Felis TMG, na kutazamia kuzinduwa albamu hii katika tamasha kabambe itakayofanyika katikati ya mwezi Julai katika mji wa Crown Point, Indiana, Marekani. Felis anasadikika kuwa muimbaji wa kwanza wa nyimbo za Injili kutoka Afrika mashariki na kati kuingia mkataba na TMG.

Felis ni mwenyeji wa Jamhuri yaki Democrasia ya Congo, mwenye nia yakufikia mataifa kupitia uimbaji wa nyimbo za injii. Akifuata wito wa Roho Mtakatifu, aliondoka nyumbani kwao katika mji wake wakuzaliwa Bakavu, nchini Congo. Alianza safari yake huku akihudumu katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Rwanda, Burundi, Uganda na kenya kabla yakufanya makazi mkoani Arusha, nchini Tanzania. Jipe Moyo, ni album ya tatu (3) yake Felis baada ya kazi yake ya kwanza iliyojulikana kama, Yuko Njiani, iliyotolewa Arusha 2006, na Yesu ni Mungu, iliyotolewa 2008.

Jipe Moyo imebeba mchnganyiko wa midundo maalum "unique blend" kutoka katika utamaduni wa Congo na Afrika Mashariki. Kwa ajili ya kufikisha Habari Njema na ujumbe muhimu na wenye thamani, unaofariji na kuleta tumaini, pia ujumbe huu ni kwa watu wa makabila na tamaduni zote popote duniani.

Felis alikuwa na hili lakusema: 

"Jipe Moyo" ni ujumbe maalum Mungu anao sema na ulimwengu kwa sasa. Katika mambo yote haya yanayoikumba dunia, watu wanakata tamaa, hawajui hata lakufanya au pakwenda. Kama wewe pia unapitia hali ya kukataliwa na ndugu jamaa na marafiki, au kukosa kazi na kufukuzwa kazini, ugumu wa maisha au ugumu wakufikia malengo. Ujumbe wake Mungu kwako leo ni huu, "Jipe Moyo!"

Comments