Tuesday, June 9, 2015

Rais wa Zanzibar aongea na Watanzania UjerumaniRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein ameongea na watanzania katika mkutano na Diaspora uliofanyika Würzburg nchini Ujerumani. Mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V, ulifanyika katika Hotel ya Maritim Hotel mjini humo mida ya saa 10 alasiri. akianza kwa kufungua mkutano huo Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Bw. Philip Marmo ,alisema, watanzania wanaoishi ujerumani wanaishi bila ya kuvunja sheria nchini humo, na wanampa Mhe Balozi  Marmo faraja kubwa kwani hajawahi kusikia Mtanzania yoyote Aliye Jela au Aliye na kesi ya aina yoyote ile tangu afike ujerumani, taarifa alizonazo ni kwamba Kila mtanzania anafanya  shughuli zake za kujitafutia riziki iliyo halali. Bw. Marmo  alimpongeza sana mwenyekiti wa umoja wa Watanzania ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuendesha Umoja huo na kuwasiliana na Ofisi ya Ubalozi mara mtanzania anapopatwa na shida ya aina yoyote ile. naye mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani U T U e.V Alieleza kwa ufupi  madhumuni ya kuanzishwa Umoja huo ambayo kwanza ni kukusanya watanzania na kuwa pamoja na kusaidiana katika shida kwani miaka ya nyuma watanzania walikuwa wakipata shida nyingi laiki kwa vile hapakuwa na chombo kinachowaunganisha ilikuwa ni tabu kujua nani na ana shida gani, aidha alieleza kuwa UTU e.V ni chombo ambacho kitakuja kuwajenga watoto wa  kitanzania ambao wanazaliwa Ujerumani katika kujua wapi walipotokea na wana fursa zipi ndani ya Tanzania. alifafanua kwamba  watanzania waliokwenda ujerumani wakiwa watu wazima wanajua nini cha kufanya ili kupata fursa zilizopo Tanzania lakini watoto waliozaliwa ujerumani labda watakosa mawasiliano na ndugu zao waliopo Tanzania hivyo  Umoja wa watanzania Ujerumani kitakuwa ndio chombo chao kitakachowaunganisha baina yao.

Naye Mhe Rais wa Zanzibar Bw Ali Mohammed Shein alimalizia Hotuba yake kwa kuwaasa watanzania wanaoishi Ujerumani wakae kwa amani na waendelee na shughuli zao za kujitafutia riziki ya halali, aidha alisema Serikali ya tanzania inapata faraja kubwa kuona Watanzania wanaishi nje ya nchi bila ya kupamatatizo wala kusababisha matatizo, aliwaasa Watanzania kuheshimu sehemu zao za kazi, ajira zao na kuzinyenyekea kwani sehemu mtu anayopata riziki inapaswa inyenyekewe na kuheshimiwa, kabla ya kufunga mkutano huo uliohudhuriwa na Watanzania wanaoishi ujerumani kutoka miji mbali mbali nchini humo, Mheshimiwa Rais Wa Zanzibar aliwaambia watanzania wasifikirie kuwekeza Tanzania bara peke yake kwani hata Zanzibar ni kwao hivyo wanakaribishwa wakati wowote

No comments:

Post a Comment