MBIO ZA UBUNGE MOSHI MJINI,KWA NINI ? KIJANA DAUD MRINDOKO VUTIO LA WENGI!

Daudi Mrindoko Kijana mwenye umri mdogo kuliko wagombe wote Kilimanjaro

Moshi Town,

Katika mbio za kuelekea uchaguzi mkuu 2015, katika jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro jina la kijana Daudi Babu Mrindoko (30) aka Obama wa moshi limekuwa kivutio na gemeo la wapiga kura jimboni humo,tena kivutio na gemeo la wapiga kura wote kuanzia wazee na vijana,wanawake na wanaume kuanzia chama chake cha CCM hadi vyama vingine ! jina Daudi Mrindoko ndio gumzo la wakazi wa Moshi Mjini kuelekea uchaguzi mkuu 2015 kuwa wakazi hao wamesikika na kufunguka kwa uwazi kuwa watampigia kura kijana huyo bila kujali atagombea kwa tiketi ya chama gani !
Kwa nini ? Daudi Mrindoko baadhi ya wakazi wa Moshi mjini wanafunguka kwa
kumtaja kijana huyo ndio tegemeo lao kwa sababu kuwa ni mtoto anayejua hali halisi,umri wake na harakati zake ni vipimo hai kabisa kuwa ndio dira ya kuwalekeza wakazi wa Moshi katika kujikwamua katika kero za maisha zikiwemo kushuka kwa kiwango cha elimu jimboni humo,uchumi ambao wakazi wa mosho mjini wengi wao utegemea biashara ndogo ndogo ,wakiwemo waendesha boda boda, Kero za ulinzi
"Kwa sasa jiji la Moshi  linasumbuliwa na wizi wa maji ,vibaka wanaunganisha mabomba ya maji kwa njia za ujanja" ikumbukwe pia soko kuu la Mjini Moshi lilifungwa kwa muda zaidi ya mwaka moja na kusababisha kudondoka kwa uchumi wapiga kura wa jimbo hilo na kuwafanya wanyanyasike kama vile sio binadamu huru!
Daudi Mrindoko aliyeshawishiwa kwa nguvu kubwa za wakazi wa Moshi achukue
fomu za kugombea ubunge na yeye mwenyewe alikubali kwa kusema ameshawishika na ataomba fomu wakati ukifika kwa tiketi ya CCM,pia alifunguka kwa kusema iwapo akipewa fursa na chama chake,basi lengo lake ni kuifanya Moshi Town kuwa Geneva kwa kuanza na wito kwa wenyeji wa Kilimanjaro kushiriki katika kuijenga Moshi town baadala ya kukimmbilia ktika mikoa mingine.
Daudi Mrindoko ndiye mtia nia mgombea mwenye umri mdogo kuliko wagombea wote mkoa Kilimanjaro,Daudi Mrindoko mwenye umri wa miaka 30 ni mjumbe wa UVCCM mkoa Kilimanjaro,Mwenyeki wa taifa wa UMOJA WA WAZALENDO TANZANIA(UWAWATA) mwanaharakati mtetezi wa wanyonge aliye mstari wa mbele wakati wowote.

Comments