Maonyesho ya Wurzburg Festival Ujerumani,Yavamiwa na mafuriko ya maji

Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni waponea Chupu Chupu !


wafanya biashara


Wurzburg,Ujerumani,

Jumamosi ya tarehe 1 Juni 2013,katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival,
Kulikuwa na machonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea
miaka 25.
Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na
mashaka baada ya wanii wa Ngoma Africa band aka FFU,kutoweka ghafla katika
chumba cha kubadilishia nguo (back Stage) na kutojulikana waliko, wasi wasi ulitanda labda watakuwa wamezolewa na mafuriko ! Lakini baada ya masaa kadha
watayarishaji waligundua kuwa mkuu wa bendi hiyo field-marshal Kamanda Ras Makunja alikiondoa kikosi chake baada ya makachero wa bendi hiyo maarufu kama "Anunnaki Empire" kumtonya boss wao kuwa eneo la festival sio salama
mto ulio jirani wa eneo hilo  unajaa maji kwa kasi,Kamanda bila kuaga kawatoa FFU
wa Ngoma Africa band katika hali ya usiri na kuwanusuru vijana wake, na simu ya ke ikazimwa hadi baada ya masaa fulani ndipo ikawashwa na kuwajulisha waandalizi wa onyesho wasiwe na shaka kamanda na kikosi cha Ngoma Africa band wapo salama kambini,kitendo hiko kiliwaacha midomo wazi baadhi ya wadau ! wengine kudiriki kusema kuwa Simba ni Simba.
Wadaku wametonya kuwa tamasha hilo lilianza mwishoni mwa mwezi mai siku ya ijumaa 31.Mai 2013 kukiwa na maelfu ya watu na wasanii mbali mbali walioalikwa
wakiwamo mkongwe Manu Dibando,Alfa Blondy,Salifu Keita ndio walioanza kufungua dimba, Ijumaa hiyo hali ilikuwa shwari lakini ilipofika jumamosi hali ya hewa
ilianza kubadilika kwa mvua na upepo,wasinii wengine wakiwa kwenye vyumba vya kujitayarishia miongoni mwao wakiwamo "Ngoma Africa band " a.k.a FFU Ughaibuni, baada ya hali ya hewa kuanza kubadilika kwa upepo na mvua ndio
inasemekana kuwa  Kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa band,
Kuondoka katika eneo la festival (eneo la hatari) lilikumbwa na maji,katika
mazingira ya ajabu. Watonyaji wa habari wamedai kuwa walitoroshwa kwa magari
mawili meusi aina ya van yalikuwa na madilisha ya kiza (tinted windows).Kamanda Ras Makunja
kateleza kama nyoka na kikosi chake.
Mafuliko hayo yamevamia pia baadhi ya miji nchini Ujerumani na ulaya ya mashariki ka kusababisha vifo vya watu 12.