UMOJA WATANZANIA UJERUMANI (UTU) Inawakaribisha katika SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA


Mjini Koloni, Ujerumani
Jumamosi 27.04 .2013

Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo anayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na marafiki  wa Tanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 Za mchana  hadi usiku wa manane.

Katika sherehe hio ambayo  imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik,  kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania,  na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. Ngoma za asili kutoka Tanzania, Mwanamuziki Kongwe Bi.Tabia Mwanjelwa naye atakuwepo,  Msanii wa Bongo Flava Shah Smooth mwenye maskani yake  Dublin,. Kikundi cha Sarakasi kitafanya mavitu yake Live ! na  mwisho watanzania na wageni wote watapata Fursa ya Kuduarika na midundo  kutoka Tanzania kupitia DJ Sudi Mnete wa Deutschwelle.
Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya maazimio ya U T U la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Ulaya. Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha  pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni,
Umoja ni Nguvu!
KARIBUNI SANA MJINI KOLONI

Comments