KUTOKA USWAHILINI HADI UGHAIBUNI !


Sensei Rumadha Fundi (Romi) mtaalam wa ngazi za juu wa karate na Yoga ,

Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi
hatuwezi kulikwepa,mtanzania mwenye makazi yake nchini marekani,kabla ya kujikita kule marekani alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanakaki,Dar chini ya mwalimu wake
Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), baada ya hapo akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark,
akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga,Vipaji hivi vya Karate na Yoga ,Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga 
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha Fundi (Romi)( 3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.


Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.

Comments