Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Zenno Ngowi akiongea
wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 3 ya Tanzania Homes Expo yanayotarajiwa
kufanyika Juni 2013. Kushoto ni mratibu wa maonyesho hayo Happy Geddi na
kushoto ni Meneja Masoko Mesha Gobba.
Maonyesho
ya tatu ya Tanzania Homes Expo yanatarajiwa kufanyika Mlimani City Juni 2013 na
kushirikisha makampuni pamoja na taasisi mbalimbali za sekta ya nyumba Tanzania
na Kenya. Mara ya mwisho maonyesho hayo yalifanyika Desemba 7 hadi 9 2012.
Akiongea
na waandishi wa habari wakati akitangaza kufanyika kwa maonyesho hayo,
Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, ndugu Zenno Ngowi alisema, “Katika maonyesho
hayo, watoa huduma wa sekta ya nyumba kama makampuni ya nyumba, wachora ramani,
bima, makampuni ya ulinzi, mikopo, bima, wakandarasi na wengine wengi watapata
fursa ya kuelezea huduma wanazozitoa.
Tanzania Homes Expo, itazialika
taasisi zinazohusika na ujenzi kushiriki kwenye maonyesho yajayo ili kutoa
elimu kwa uma. Kuna msemo maarufu usemao ‘’kutokujua sheria haihalalishi
kutenda kosa’’. Kwetu sisi tunaamini Tanzania Homes Expo inatoa fursa nzuri kwa
jamii yetu kupata taarifa na kujua masuluhisho mbalimbali ya ujenzi”.
Kuhusu ushiriki wa makampuni kutoka
Kenya, mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Bwana Zenno Ngowi alisema “Tunaamini
kupanuka kwa wigo wa washiriki toka kwenye Nchi ya jirani kutatoa fursa ya
Wananchi kupata masuluhisho mbalimbali ya ujenzi.
Nishati mbadala, ni eneo jingine
ambalo tunategemea kupata washiriki wengi wapya ambao watakuja kuonyesha masuluhisho
mbalimbali ya nishati mbadala”.
Kwa taarifa zaidi au kushiriki
tembelea tovuti; www.eaggroup.co.tz au tuma barua pepe info@tanzaniahomesexpo.org
Comments
Post a Comment