Tuesday, July 26, 2016

Ngoma Africa band yawapandisha mzuka washabiki mjini Tübingen,Ujerumani

Na Zainab Ally Hamis
Dar es salaam School of Journalism(DSJ)

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band almaarufu kwa majina ya FFU-Ughaibuni au viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens wengine wanawaita "Watoto wa Mbwa" juzi jumamosi 23 julai 2016 walifanikiwa tena kuwatia kiwewe na kuwapandisha mzuka washabiki katika maonyesho makubwa ya International Afrika Festival mjini Tübingen ,ujerumani.mkuu wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja alikiongoza kikosi kazi chake jukwaani wakiwemo washambuliaji wa magitaa au mitutu akina afande Chris-B, na Professor Matondo Benda,mpiga bass Aj Nbongo na drumer Sajent major Jo Jo Sousa,safu ya waimbaji na wanenguaji wa kike akina Jessicha Ouyah na Flora William bendi hiyo ilifanya vitu vyake jukwaani na kuwatia kiwewe washabiki

No comments:

Post a Comment