Wednesday, July 27, 2016

KUFANIKIWA KATIKA MAISHA SIO ELIMU BALI UJASIRI WA KUJIAMINI NA KUTHUBUTU


Nimepata huu ujumbe toka kwa rafiki kupitia chat ya whatsapp. Sijajua nani ameandika ujumbe huu ila nampa hongera 100%. Kuna wakati maisha ya elimu yalikuwa yanadisappoint maana kwa mtu mwenye uchu wa maendeleo niliona kama vile nachelewa sana, maana nasoma miaka mingi halafu umri unazidi kwenda na bado ukiomba kazi unaambiwa tunahitaji experience ya miaka flani au flani.
Kama sio kutupa msongo wa mawazo na kutufanya wajinga ni nini? 

Ila pia nashukuru Mungu kwa mkwamo huo kwasababu ulinilazimu kutoka nje ya elimu ili kutafuta maisha. Elimu ni sehemu moja tu ya maisha ya mtu, kuna sehemu nyingine ambazo ni talanta ulizopewa na mwenyezi Mungu, mapenzi yako mwenyewe katika jambo flani, uzoefu wa kufanya jambo flani kwa muda na mengine, hayo yamekuwa sababu ya kutupatia kipato sisi tuliokerwa na habari za "work experience".

Kama mtu alikua anasuka nywele wenzake wakati yupo shule ya msingi au sekondari, unakuta huyo mtu hata kama ana shahada ya ualimu na kazi hapati basi atafungua saluni yake ilimradi tu ajipatie pesa maana atleast ana ujuzi wa jambo flani kwa muda mwingi wa maisha yake.
Huu ujumbe pia uwape motisha wasiokuwa na elimu ya juu, watafanikiwa tu, wasikae kujutia kukosa elimu wakati Mungu amewapa talanta na kuwawekea mapenzi ya fani flani ndani yao au wamekua wakifanya jambo flani lililowapa ujuzi na baadae wanaweza kugeuza ujuzi wa jambo hilo kuwa ajira.
                               
   'BE INSPIRED'

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!).

Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana. 

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

Hii inachangiwa na mambo mawili.

1 - Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.
Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio.

Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2 - Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani.

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze.

No comments:

Post a Comment