ALIKIBA's interview with Sporah



Hey y'all. 

I'm not much to comment on things coz i usually think my comments are harsh. Ila baada ya kuangalia hii video nimeona nicomment tu. 

I like Sporah and her show, napenda research zake before interviews, etc. Ila hii interview imenifanya nijiulize maswali mengi, moja wapo ikiwa ni KWANINI wabongo tunapenda kushindanisha watu? Niliona comments za watu mitandaoni but sikutaka kusema lolote coz sikuwa nimeona hii interview, ila baada ya kuiona nimeelewa kwanini watu wengi wamechoshwa na hii tabia ya kushindanisha watu. 

Wabongo tukubali kuwa kila mtu ana nafasi yake kwenye industry ya music and entertainment. Kila mtu anaimba kivyake, kila mtu anakitu chake pekee kinachomfanya ku "stand out". Kila mmoja ameleta mabadiliko flani kwenye industry. Kila mtu apewe heshima yake. 

Swali langu kwa jamii yetu ni hili; kusema nyimbo zote za bongo kuitwa bongo flava, je hilo ndio linalowachanganya watu na kutaka kila mtu ashindanishwe na mwenzie? ama kuna jambo lingine?

Nimeuliza hivyo kwasababu, kama tukiweza kuivunja bongo flava kwenye vipengele tofauti then nina uhakika kila msanii anasimama katika aina yake ya mtindo wa kuimba. Kwa mfano, kuna aina mbali mbali za muziki kama vile, POP, RnB, HIP HOP, JAZZ, CLASSIC, DANCE, TECHNO, na list inaendelea. Huezi kuta hata siku moja ukamshindanisha Jay Z na msanii mwingine ambaye haimbi HipHop kisa wote wametokea Marekani. Pia huwezi kumshindanisha Jay Z na Lil Wayne kisa wote wanaimba HipHop, wakati wote tunajua kuwa style zao za kuimba ni tofauti sana.  (I HOPE KWA HUO MFANO TUKO PAMOJA) 

Pia wenzetu wanakitu kinaitwa Legends, kwa bongo, zaidi ya wale walioimba enzi za babangu na mamangu, sijui kama watu wanatoa heshima kwa wasanii wengine na kuwaita legends. Kuna wasanii kama Lady Jay Dee, Professor J, AY, Dully Sykes and the list goes on and on, hao kwangu mimi ni legends kwenye bongo flava. Wameleta mabadiliko sana kwenye muziki wa kizazi kipya wa Tanzania. Isije hata siku moja mtu akawadharau eti kisa kuna msanii miaka ya sasa ambaye anatengeneza pesa nyingi zaidi yao. Status ya kuwa legend haifi kamwe. 

Pesa isiwe sababu ya kusema nani ni mkubwa kuliko mwingine. Status ya mtu katika industry itokane na sehemu yake aliyocheza katika kuleta mabadiliko flani, au jinsi alivyoanzisha kitu kipya, etc. Mfano mzuri ni Angelina Jolie, wote tunamjua na tunapenda movie zake na pia tunamkubali, ila kamwe hakuna mtu atakayesema Angelina Jolie amempita Marilyn Monroe. Wote wana nafasi zao kwenye industry hata kama sasa Angelina anapokea hela nyingi kuliko alizowahi kushika Marilyn Monroe wakati wa uhai wake. 

https://www.youtube.com/watch?v=dVwMuAdqzTg kwenye hii link utaona sehemu (dakika 27:59) inayosema Usher aliuza album ya Confessions ikawa one of the biggest selling albums since album ya Michael Jackson ya Thriller, but i guarantee you MJ alibaki na nafasi yake na Usher amebaki na nafasi yake, pesa, mauzo ya album, kufanya shows dunia nzima, na mengineyo mengi, hayawezi kumfanya Usher awe mkubwa zaidi ya MJ. 

JAMANI, TUWAACHE WASANII WETU WAFIKE MBALI. TUSICHOCHEE UGOMVI (UNLESS MTATUMIA HUO UGOMVI KUNUNUA KAZI ZAO WOTE HALAFU MKAFANYE COMPARISON ZA KAZI ZAO HUKO MAJUMBANI KWENU). 

KITU CHA MWISHO: MSISAHAU HAWA WATU NI BINADAMU, HIZO COMMENTS MNAZOZITOA ZA KUMPONDA MTU BILA KOSA ETI KISA MSANII MNAYEMPENDA HAJAMPENDA HUYO MTU, SIO POA. KABLA HAMJAWATUKANA AU KUWASEMA VIBAYA, NAOMBA UWAZE UNGEJISIKIAJE KAMA HUYO MSANII ANAYESEMWA NI KAKAKO, BABAKO, MTOTO WAKO, NDUGU YAKO, AU WEWE MWENYEWE. HAMKATALIWI KUMPENDA MTU, ILA MSIM 'CONDEMN' MTU KWA KUMFAIDISHA MTU MWINGINE AMBAYE HAKUSAIDII KWA NJIA YOYOTE KATIKA MAISHA YAKO HUKO NYUMBANI KWAKO, HAKUPI PESA, HAKULISHI, HAKUPI NGUO, HATO KUFA KWA AJILI YAKO. LET THEM BE!!!!

SUPPORTING TANZANIAN MUSIC & ENTERTAINMENT. #HOME

Comments