Usipocheka hujui kusoma

Nimeamka leo nikaona msg from my mdogo called AJ..nilicheka mpaka usingizi wote ukaisha.

Enjoy!

Mimi naitwa Gloria, tunakaa Boko,
zamani tulikuwa tunakaa Magomeni sasa
baba alipopata hela za kustaafu
akajenga huku Boko ndio tumehamia.
Nimemamliza fom six niko nyumbani
nangoja majibu. Kuna kitu naomba
mnisaidie.

Tarehe 1 April nilimwambia baba yangu
kuwa nimechaguliwa kujiunga na chuo
kikuu cha Oxford Uingereza. Baba
alifurahi sana akaagiza kuku wawili
wachinjwe na mama apike pilau. Baada
ya hapo kila siku amekuwa akirudi
nyumbani kalewa anaimba kuwa
mwanae ninaenda Uingereza. Juzi
nimegundua kauza kipande cha ardhi
jirani na kwetu ili aanze kukusanya
fedha za mimi kuishi Uingereza. Pia
nasikia ameshakopa hela Saccoss ili
ajumlishe kwenye nauli yangu ya
kuendea Ulaya. Pia alitoa shilingi laki
tatu kanisani kama sadaka ya shukrani
kwa mimi kuchaguliwa kwenda
Uingereza. Mzee naomba unisaidie
ntawezaje kumwambia baba kuwa siku
ile nilikuwa namtania ilikuwa sikukuu ya
wajinga?

Naomba msaada haraka au nitoroke
kwetu?

Comments