joke


Jamaa wamejificha mahali wanavuta bangi zimewakolea kichwani tayari ghafla simu ikaita, mmoja akapokea.
Kwenye simu binti: Sema baby.
Jamaa: Hello darling.
Binti: Darling niko town shopping na nimeona viatu vya ngozi hapa wanaviuza elfu 80, naweza kuvinunua mpenzi?
Jamaa: Hawaezi kukupunguzia hiyo bei?
Binti (kwa sauti ya furaha): amesema anaweza nipunguzia elfu kumi tu, ataniuzia elfu 70.
Jamaa: basi sawa, chukua fasta kabla hajabadili mawazo.
Binti: Thanks love! Na baibe kuna gauni nimeona linauzwa elfu 60 halafu wanakupa na Nivea for men! I promise usiku ntakusapraizi!
Jamaa: sawa my dear, si utanifanyia kabisa massage na hiyo Nivea nifurahi kabisa.
Binti: sawa mpenzi! Kitu kingine dear, nina ATM card yako hapa,si nitumie tu honey? Please baibeeee!
Jamaa: Oh mpenzi, ni sawa baibe tumia but usizimalize hela yote.

Click. Akakata simu. Marafiki aliokuwa anavuta nao bangi wakaanza: Ayaaaaaah! We jamaa mbulula! Umelogwa, wala si bure!? We umekuwa ATM machine ya huyo binti au boifrendi! Mteme, hana maana huyo, atakufilisi!

Jamaa kwa tabasamu akajibu: hebu tulieni kwanza ... hivi hii simu ni ya nani? Yangu iko mfukoni!

Comments