Monday, January 19, 2015

Msiba Ujerumani

Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.

Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla.


Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin!Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:Diana Kajuna
IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
BIC: GENODED1BRS
Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eGTunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:e-Mail: IMajura@aol.com
Germany

No comments:

Post a Comment