MTB: MAMBO?
Deborah: Poa
MTB: POLE NA HONGERA KWA SHUGHULI
ZA MAISHA.
Deborah: Asante sana. Namshukuru Mungu.
MTB: KWA FAIDA YA WASOMAJI, NAOMBA
UTUAMBIE JINA LAKO KAMILI
Deborah: Jina langu la ubatizo
naitwa Deborah Vicencia Myren Kerenge
MTB: JINA LAKO LA USANII JE?
Deborah: Najulikan kama Candy a.k.a
Mama Msaliti
Deborah: Ila ukitaja tu Candy kila
mtu anajua ni Nani.
MTB: HAHAHAHA...SAWA.
Deborah: (smiling)
MTB: MAJINA YAKO YA USANII
UMEYAPATAJE?
Deborah: Jina la Candy lilianza
kwenye group inayoitwa AFRICAN YOUTH ya Norway. Tulikua
wadogo tukiingia studio kila mtu anajibatiza jina lake la kurap,na mimi
nikaandikaga wimbo unaitwa they call me C.A.N.D.Y tangu siku hiyo nikaanza
kuitwa Candy mpaka Leo kuna wasio Lijua jina langu la ubatizo.
Deborah: Mama Msaliti nilipewa na
Christian Bella baada yakuwepo kwenye Video
yake inayovuma sana nchini Tanzania
(MSALITI).
MTB: SAWA.
MTB: NAOMBA UTUPE HISTORIA YAKO YA
MAISHA KWA UFUPI, KAMA VILE UMEZALIWA WAPI MPAKA SASA UNAFANYA NINI.
Deborah: Bila shaka.
Deborah: Nimezaliwa miaka ya 80 Nakitu
Musoma Tanzania,ni mtoto wa pili katika familia. Nina dada mkubwa na wadogo
wanaonifuata.Nimeishi na kusoma Dar pamoja na Iringa Tosamagang.Nilivyofika
miaka 13, kama sikosei, nikahamia Sweden /Norway. Kwa sasa ni Psychiatric
nursing Assistant. Nabado ninaendelea kusoma Sweden.Vilevile mimi ni mwanamke
ninaependa kujituma kwahiyo i'm a business Woman nauza vitu mbalimbali
nakujishungulisha na mambo madogomadogo apart from my job.
MTB: HONGERA KWA KUWA MTU
ANAYEJITUMA
Deborah: Shukran shukran.
MTB: SABABU KUBWA YA INTERVIEW HII
NI TETESI NILIZOPATA KUWA UNAHAMA FANI, KUTOKA KUWA VIDEO VIXEN NA KUWA MSANII,
JE NI ZA KWELI?
Deborah: Kwa furaha moyoni napenda
nikwambie kua ni kweli kabisa.
MTB: UNAIMBA STYLE GANI YA MUZIKI?
Deborah: Mimi ni mpenzi wa Reggae Zouk
na vilevile Old school HIP HOP. Kwa sasa wimbo ambao
utatoka hivi karibuni ni wa HIPHOP umekaa kisexysexy flani siunajua tena swaga
flani hivi amazing. Na mwingine ambao naufanyia
kazi upo studio Jamaica ni Zouk imemix na reggae.
MTB: HAHAHAHAH, SAWA.
MTB: MPAKA SASA UMEANDAA NYIMBO
NGAPI?
Deborah: Nimeandaa Nyimbo mbili
mpaka sasa.Sema huwa ninarecord then
naacha but sasa niko tayari na nina amini nimewiva, uwoga kwisha. So nawaahidi
mambo mapya na mazuri katika muziki wakiafrica.
MTB: TUNAKUSUBIRI KWA HAMU
Deborah: Asante, very soon mtaniona.
MTB: JE UMESHIRIKISHA MSANII
MWINGINE YEYOTE KWENYE HIZO NYIMBO MBILI ULIZOZIANDAA?
Deborah: Yes kwenye wimbo wa Hiphop
unaotoka hivi karibuni nimemshirikisha mwanamziki aitwae Puzzo known as blackcurtains na ni Producer mzuri sana
anayefanya kazi na wanamuziki wengi sana hapa Sweden.
MTB: LINI TUTEGEMEE VIDEO ZA KAZI
ZAKO? NA JE UNAFANYA VIDEO SHOOTING SWEDEN?
Deborah: Nisingependa kutaja mwezi
siku wala tarehe. Siunajua mambo mazuri
yakiwa Suprise ndio fresh. Ila mjue ni anytime from now. Kuhusu video Ya Hiphop
inafanyika huku huku Sweden, zifuatazo ninafanyia Jamaica na homeland Tanzania.
MTB: TUNAZISUBIRI KWA HAMU.
MTB: JE NI MSANII GANI WA TANZANIA
UNGEPENDA KUFANYA NAE KAZI?
Deborah: Kwa HipHop ningependa
kufanya kazi na Mwana F.A,Zouk ningependa kufanya na Alikiba na Christian
Bella.
Deborah: Bila kusahau kuna wimbo wa
bongo flava ambao ntafanya na BabyJ nishukapo Tz.
MTB: KUNA TETESI KUWA ULE WIMBO WA DULLY
SYKES WA BABY CANDY AMEKUIMBA WEWE, JE KUNA UKWELI WOWOTE?
Deborah: Kiukweli Dully
nimeshakutana nae na alisema wimbo kaniimbia mimi sasa nivigumu mimi kuingolea
nafsi yake kama nikweli au sio.Ukweli anao yeye Dully (smiles).
MTB: HAHAHA, SAWA.
MTB: KWA VIDEO UTAZOFANYA TANZANIA,
DIRECTOR GANI UNGEPENDA KUFANYA NAE KAZI?
Deborah: Kwasababu sijafika Tz muda
mrefu sana nivigumu kusema ila so far namkubali Nisher, Adam Juma na Jerry Mushala.
MTB: UNA UJUMBE GANI KWA MASHABIKI
WAKO?
Deborah: Wazidi kuniamini kama
wanavyoniamini na wazidi kunipa moyo ili niendelee kufanya vizuri.Naahidi kuwaburudisha
ipasavyo nasitowalet down
MTB: ASANTE SANA KWA INTERVIEW
Deborah: Nashurukuru pia.
MTB: TUNASUBIRI KAZI ZAKO KWA HAMU.
Deborah: Hivi karibuni mtafurahi.
Comments
Post a Comment