Friday, October 10, 2014

LOL

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema hivo?
Mtoto: Nina akili...


Basi mwalimu kamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya....

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?
Dogo: Yatabaki 19.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani kwa nini?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu.


Author: unknown

No comments:

Post a Comment