Wednesday, July 2, 2014

Wasanii wengi wa Tanzania kushiriki International African Festival Tubingen,Germany 2014

Habari zipenya katika vianzo kuwa wasanii wengi wa Tanzania wanatarajiwa
kufunika katika maonysho makubwa mbali mbali nchini Ujerumani katika msimu wa joto.
baadhi ya wanamuziki waliopata bahati ni pamoja na kikundi cha ngoma ya Baikoko kutoka mkoani Tanga.
Wengine ni mwanamuziki nguli wa reggae Jhikoman & Afrikabisa band kutoka Bagamoyo mkoa Pwani ambaye amealikwa rasmi na Afrikative Organization
kushiriki onyesho kubwa la International Africa Festival Tubingen 2014 yanayo anza 17 mpaka 20 julai 2014 huko Tubingen,Ujerumani.

Wazee wa kazi Ngoma Africa band aka FFU aka Anunnaki Alien,ukipenda waite "Watoto wa Mbwa" bendi isiyo kaukiwa na habari inayoongizwa na kamanda mkuu FFU Ras Makunja wao kama kawaida yao kila mwaka wanajikuta wakiwa na kazi moja tu ya kupeleka mashambulizi katika kila jukwaa kuhakikisha washabiki wao wanaokadiliwa idadi ya milioni 50 duniani wapati usingizi.

No comments:

Post a Comment