Tuesday, August 13, 2013

FFU wa Ngoma Africa band wamechukua tena International Diaspora Award 2013 Bendi bora ya kiafrika ulaya.

Si nyingine bali Ngoma Africa band aka FFU ilifanikiwa kuutetea ubingwa wake wa bendi bora na kujichukulia Tuzo ya kimataifa ya IDA kule mjini Tubingen,Ujerumani katika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.
Bendi hiyo maarufu kwa kuwatia kiwewe washabiki na mdunduko wake imevunja rekodi kwa kuwa na washabiki wa kimataifa kila pembe.
Katika maonyesho ya International African festival 2013,yaliyofanyika mjini Tubingen,ujerumani Ngoma Africa band imekubalika sio na washabiki tu bali pia
mabalozi kutoka nchi mbali mbali za kiafrika nchini Ujerumani ! bendi
Tusikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com