DAUDI MRINDOKO KASHAWISHIKA NA KAKUBALI OMBI LA WANANCHI WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUGOMBEA UBUNGE 2015
Yafuatayo ndio maelezo yake haya:
"Kwa nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu anawezesha yote na kutujalia uhai
Waheshimiwa Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama zangu na wanadau wote wanaoishi Moshi na wenyeji wa Moshi walio ndani na nje ya Moshi.
Mimi mtoto wenu,mdogo wenu na Kijana wenu DAUDI BABU MRINDOKO
Nina heshima kubwa na unyeyekevu kwenu ,Pia nawashukuruni sana kwa kunishawishi niweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo
la Moshi Mjini katika uchaguzi mkuu 2015,nafasi ambayo Ubunge ! ambayo mimi
mwenyewe kwa tafsiri ya Ubunge yaani utumishi,mtetezi,msemaji, mwakilishi n.k
katika baraza la kutunga sheria na katiba yaani Bunge, na katika tafsiri hii ya majina ya kazi hii lazima mtumishi
awe mkweli,muwazi na aliyeweka mbele kwanza maslahi ya walio mchagua.
Waheshimiwa Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama zangu
Kunishawishi kwenu Kulinifanya niwe kimya kiasi na nikiwa najiuliza maswali mengi kichwani ! Lakini maswali makubwa yalikuwa 3 (a)Nashawishiwa na jamii
nichukue fomu kwa kuwa mimi ni kijana mwenywe uwezo wa kuifanya kazi hii?
(b)Nashawishiwa kwa kuwa kijana niliozaliwa na kuelimishwa na wanao nishawishi? yaani wanachi wa Moshi mjini na ndio wananitambua tabia na uwezo wangu wa kikazi.
Swali lingine nililojiuliza ni: Hivi mtoto au kijana mwenye adabu ,Nidhamu na heshima kwa wazee na wakubwa zake walikuwa katika jamii wakimteua au kumtuma kufanya kitu au jambo tena kwa faida na maslahi ya jamii,itakuwa vema kijana huyo akatae? au asikubali kutumwa huko?
Baada ya kujiuliza mashwali hayo na mengineyo nimepata jibu ambalo:
NAKUBALI WITO WENU NA USHAWISHI WENU
Kuwa nitachukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge 2015 jimbo la Moshi Mjini.
Mmenishawishi nami nashawishika na kuthubutu kuchukua fomu ya kugombea ubunge,kwa kuwa siwezi kuwa mvunjifu au mtovu wa adabu
kukataa wito na ushawishi wenu ambao
wazee wangu,vijana wenzangu,mama na baba zangu wa Moshi mjini
mmeniteua kwa kunishawishi niweze kuja kuwa mtumishi wenu mbunge.
Kwa kuwa mmenizaa,mmenilea ,mmenisomesha mpaka elimu ya juu
na mmenishawishi kwa kuwa mnaniamini mimi ni mmoja wenu katika
maisha ya kila siku katika jamii yetu Moshi,yanafahamu wazi mahitaji yetu,kero zetu na kipi jamii yetu haitaki na kipi? Jamii yetu inataka hapa jimboni Moshi Mjini,Marekebisho gani ?yanatakiwa hapa Moshi mjini
ili palete tumaini jema na maana kamili wa wakazi wote jimboni hapa
Nayafahamu yote.
Nanyi mmemshawishi Kijana Daudi Babu Mrindoko,mtoto wenu
kwa hakika mmetuma mtumishi anayeguswa na yanayowagusa,
anayekerwa na yale mnayokelwa ! anafurahishwa na yale mnayofurahia
Kwa ni mwenzenu katika jamii jimboni Moshi mjini.
Nawashukuruni sana na Asante sana kwa Kunishawishi,Nimeshawishika
Nangojea wakati ukifika nami nifuate taratibu zote za kuchukua fomu kupitia
Chama tawala"
"NAKUBALI NITACHUKUA FOMU 2015,KWA NIA YA USHIRIKIANO WETU TULETE MABADILIKO MOSHI MJINI YENYE MASLAHI KWA WOTE"
Mungu Ibariki Tanzania
Usikose kujiunga nae at www.facebook.com/mrindoko. mwidadi
Comments
Post a Comment