Movie yoyote lazima ipitie hatua tano:
1. Development:
Hapa ni hatua ya kwanza: Uvumbuzi wa wazo/kisa, ununuzi wa hakimiliki ya idea,
Uandishi wa Script na pia pia lazima ijulikane pesa za kuwezesha shughuli
zitapatikana wapi.
2. Pre-production:
Maandalizi ya kushoot yanaanza kufanyika, waigizaji wanakodiwa na location
zinawekewa booking.
3. Production:
Shooting
4. Post-production:
Hapa ni eding ya clips/footages, photographies, sounds na visual effects, vyote
vinawekwa pamoja.
5. Distribution:
Movie inatoka, inasambazwa na kuanza kuonyeshwa.
Sasa namba 1,2,3 na 5 Africa, East Africa na
Tanzania kwa ujumla zinaweza japo pia ubora hauzingatiwi, yaani mambo
yanapelekwa kienyeji, kikujuana ( hili ni mojawapo ya tatizo la kuona actors
wale wale), pia unakuta movie au hatua hizi ni kazi jeshi la mtu mmoja! (hapa
hatuwezi kulaumu kwasababu ufinyu wa bajeti/umaskini wetu unachangia).
Kwa ulaya, kampuni ya filamu au mhusika mkuu
behind the project huwa mara nyingi anachukua mkopo benki, utambue kuwa % kubwa
ya bajeti za movie za hollywood zinakuwaga funded na banks, halafu wanakuja
kulipana baadae. Kibongo bongo tutasubiri sana kwenye hatua hii, maana hao
madirector/maprodyuza wenyewe CV zao hazieleweki na elimu upande wa film
production haitolewi ipasavyo vyuoni, so wengi ni self-made.
Tuje kwenye kipengele namba 4: hatua hii ndio
kuzungumkuti, na Hollywood ndo wameinvest hapa kuliko popote kwenye film
production industry. Eneo hili lina hitaji career kibao hap katikati:
Special
Effects Artist - Kazi yake ni
kutengeneza physical effects, yaweza kuwa ni puppet/kinyago kinachofanana na
actor ili kitumike kwenye scenes ambazo actor hawezi kuigiza, mfano kukanyagwa
na treni au kupigwa ngumi na robot.
Motion
Capture Actor - Kama movie itakuwa ni
Sci-fi au Comic, huyu actor kazi yake ni kuigiza vitendo ambavyo digital actor
(animated model) ambaye atavaa uhusika wa binadamu kwenye movie (Mf: Ghollum in
'Lord of the Rings' au yule sokwe King Kong kwenye movie ya King Kong)
Modeller: Huyu ni anaye model (kuchora na kuumba kidijitali
kiumbe chochote mf: Ghollum in 'Lord of the Rings' au yule sokwe King Kong
kwenye movie ya King Kong)
Animator: Huyu kazi yake ni kumpa uhai Model mf: Ghollum
in 'Lord of the Rings' au yule sokwe King Kong kwenye movie ya King Kong),
yaani atembee, aongee, na kuigiza kama vile mtu (actor ) wa kawaida angefanya.
Compositor: Kazi yake ni kumnyofoa actor aliyeigiza vitendo vya
Model kwenye live action scene (footage/clip) na kumpachika Model mf:
Ghollum in 'Lord of the Rings'. Pia kazi yake ni kufanya integration (yaani
digital actor aonekane ni real ndani ya clip, aonekane ni kama vile alifanyiwa
shooting).
Editor: Kazi yake ni kuzikata kata clips na kuzipangilia ili
iwe ni stori, bila hatua hii hizo visual effects na special effects havina
maana: I mean yote yanafanyika kwaajili ya kupamba stori, bila stori ya
kueleweka behind the movie, umechemsha. Na ndio maana lazima uje na Movie Title
kali. Hivi we ukiskia jina la movie linasema: After Earth,
Terminator, Apocalypto, The Rise Of The Planet Of The Apes....hutaitafuta
hii movie???
Bila kusahau, hawa pia wanahusishwa kwenye
Post-Production ingawa sitawaelezea kwa leo: Graphics Designer, Motion Graphics
Designer, Visual Effect Artist, Sound Designer, Shader (kumpa kivuli Model sehemu
za mwanga), Texture Artist (kumpa ngozi Model ili awe ni real person au monster)
na Lighter (kudhibiti physics ya Model sehemu za mwanga).
HITIMISHO:
Sasa unaona hatua hiyo ni kubwa. Inahusisha
Software nyingi, ila zinazotumika Hollywood na kwenye major studio za dunia kv:
Columbia Pictures, WETA (waliotengeneza Lord Of The Rings, King Kong n.k.), MGM
na kadhalika ni Autodesk Maya (hili
ndo baba la mababa, hakuna program itakuja kupiku hii mpaka Yesu
anarudi), 3DSMax, The Foundry Nuke, Zbrush na kidoooogo Adobe After Effects,
Photoshop na Adobe Premiere au Final Cut.
Lakini hizi studio ziko mbele sana tangu miaka
yah vi karibuni kiasi kwamba zinajiandikia program zao zenyewe, maana kuna idea
zingine za movie zinahitaji science ingine ivumbuliwe. Mfano wa movie hizo ni
I, Robot.....Avatar nk.
Cha ajabu, unaweza kugrasp kidogo kidogo kwenye kila
area, hivyo ukajikuta una kuwa jeshi la mtu mmoja la Hollyhood, na ndio sababu
ya wingi wa short animated na short feature films zilizozagaa kwenye Youtube.
Ajabu ingine ni kwamba hivi vitu hufundishwi,
licha ya kuwa kuna vyuo vinatoa elimu husika katika kila kipengele, lakini to
become the best ni lazima ujifunze na kufanya practice mwenywe, hollywood stars
wote kuanzia editor, animator mpaka motion graphic designer ni self-taught.
Kwahiyo chukulia hii kitu ni kama kipaji. Nitaelezea kwa upana hili siku
nyingine.
Tuje Africa, (hapa sizungumzii kampuni za ulaya
zinazo kuja kufanyia movie Africa), nazumguzia Africa kama Waafrica na Tanzania
kama Watanzania wenyewe, tunaweza kufanya hivi ila tunakabiriwa na changamoto
ambazo ni mpaka ziondoke, au wawili watatu wajikusanye na kuvuta nguvu ndio
wanaweza kufanya angalau Action Movie, yaani filamu isiyohusisha models (hasa
wa liquid kv: maji, monster nk) na motion capture. Aina hii ya move ni kama
Transporter au movie za Steven Seagal.
Changamoto zinazotukabili ni: hatuna assets,
zinahitajika camera za adabu na super computers, nitachambua hili siku
nyingine. Pia elimu...nina uhakika hakuna film prodyuza yeyote wa Bongo
anayejua hata Interface ya Autodesk Maya inafananaje! Wengi movie zao wanatumia
Pinnacle, Premiere pro, Final Cut, Sony Vegas na kidoooogo Adobe After Effects.
Pia sijui ni uvivu ama uzembe ama ndo hawana
hata computer zenye uwezo wa kurender faster, kwasabau unakuta movie ina High
Contrast, haina Color Correction yoyote au hata Visual Effects zozote za
kuzugia, utadhani clips zimetolewa tu kwenye camera na kuwekwa kwenye computer,
editor akafanya cutting, aka export! ETI TAYARI MOVIE!!!! au hivi vitu
wanavijua sema computer zao hazina speed ya kurender vitu hivyo muhimu kwa
kila commercial video ili kusudi tu watoe na kuuza movie mpya kila
siku. Pia hata vitu vinavyotumiak wanadownload kudownload kwenye Net, mfano Sounds Effects na
Visual Effects za hapa na pale. Ninaweza kudhibitisha hili.
NDOTO ZANGU NI KUBADILISHA HII HALI, QUALITY NA
TECHNOLOGY INAYOTUMIKA KWENYE FILM/VIDEO INDUSTRY YA TANZANIA, EAST AFRICA NA
AFRICA KWA UJUMLA. NAFUNGUA KAMPUNI (LEGENDS MULTIMEDIA) KWA MADHUMINI HAYA.
MUDA SI MREFU MTAANZA KUNIONA KAM VIDEO DIRECTOR KWENYE MUSIC VIDEOS ZA WASANII
MBALI MABLI.
UWEZO, FAIR SKILLS NA JUHUDI YA KUTAFUTA CAPITAL NA ASSETS
NINAVYO. PIA NAENDLEA KUJIFUNZA HIGH-END SOFTWARES 2 (Maya na Nuke – huu ndo
moyo wa Hollywood revolution), MUDA SI MREFU NIANZE KUPRODUCE SCI-FI SHORT
MOVIES ZITAKAZONISAIDIA KUPATA UFADHILI WA KUTENGENEZA FEATURE FILMS WITHIN
TANZANIA, INGAWA HADI HAPO NTAKUWA LOCALLY ESTABLISHED NA KULETA MAPINDUZI
BONGO KUPTIA UTENGENEZAJI WA ACTION MOVIES NA HIGH-END VIDEO CONTENTS.
Michael Ngusa
+255 769 356124
michaelngusa672@gmail.com
Arusha
Comments
Post a Comment