Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U) Umezindua Mtandao wake leo hii Tarehe 19.05.2011, mjini Aschaffenburg ujerumani. Mtandao huo ambao umeaza kutumika kwa lugha ya Taifa ya Ujerumani (kijerumani) upo mbioni pia kutandaza habari kwa lunga za kimataifa ikiwemo kiswahili. Akiongea na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti wa umoja huo mheshimiwa Mfundo Peter Mfundo amewataka wanachama wa U T U na Watanzania wote kwa Ujumla kuwa na subira kidogo kwani mtandao huo utaanza kupatikana kwa lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuwapasha kila taarifa na kinachoendelea kutoka kwenye umoja wenu. Mtandao huo ambao unapatikana katika www.ututz.com au http//www.ututz.com kwa mawasiliano zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com kamati ya UTU inawatakia kila la heri katika kurambaza kwenye mtandao wetu.
Comments
Post a Comment