MANJONJO YA MWANASHERIA RWEGOSHORA.
Baada ya kumaliza degree yake ya sheria mlimani, Bwana Rwegoshora
aliamua kurudi nyumbani kwao Bukoba
mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya kuhudumia clients (wateja).
Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake, alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake.
Hapo ndipo alipoanza kunyanyua mkono wa simu ya TTCL, wakati anajizungusha kwenye kiti cha kuzunguruka.
Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha huku akiendelea kuongea na simu, alisikika akiongea ''No, no, no, Absolutely no, You tell those clowns in New York that I won't settle this case for less than one million. 'pause'
Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next week, I'll be handling the primary argument and the other members of my team will provide support. Okay.
Pliz don't forget to tell the State Prosecutor that I'll meet with him next week to discuss the details."
Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga kwa muda zaidi dakika 5.
Baada ya kumaliza kuongea na simu, bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa:-
''Samahani sana, kwa kukupotezea muda wako, unajua tena kazi zetu hizi unaumiza kichwa sana, kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani niko busy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe.
enh by the way, what can i do for you?
Jamaa alijibu.
'' Mimi ni mfanyakazi wa TTCL, nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani''...
Comments
Post a Comment