40 DESIGNERS TO LAUNCH THEIR NEW
COLLECTIONS IN DAR
PUBLIC ENCOURAGED TO SUPPORT MADE IN
TANZANIA INITIATIVES
The Sixth
annual Swahili Fashion Week will take place at Golden Tulip hotel from the, 5th
to 8th December 2013 in Dar Es Salaam, Tanzania.
Swahili
Fashion Week 2013 will collectively bring together 40 designers from within
Tanzania and beyond to showcase their collection, predicting trend for the East
African market for year 2014.
“Swahili
Fashion week this year is aimed at reaching out to the public to emphasize and
promote talents in the fashion industry. It’s more about valuing our own
designers and building brands and taking them to a different level year in year
out.” Stated Washington Benbella, Swahili Fashion Week Manager
Being the 6th year of
Swahili Fashion week, this year during the Emerging Designers Competition, the
organizers have come up with a theme called “Evolution”. Based on the theme, it
is required of the emerging talents participating to create ensembles that have
evolved, not necessarily neo but that which could be retro with an interesting
unique twist to it.
“We urge the public to support the
design industry and proudly wear MADE IN AFRICA, especially Tanzania. The local
talents need to be nurtured to evolve them into synonymously globally recognised
Brand names. Charity begins at home, thus we look forward to support from local
companies and organisations to facilitate the trade of business of fashion”
stated Hamis K Omary Business Development manager
Swahili
Fashion Week and Awards 2013 is sponsored by EATV, East Africa Radio, Push
Mobile, Golden Tulip Hotel, BASATA (Baraza La Sanaa La Taifa), Ultimate
Security, Global Outdoor Ltd, Eventlites and 361 Degrees.
NOTE TO
EDITORS
ABOUT
SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion
Week is THE largest and biggest fashion platform
in East and Central Africa for fashion and accessory designers from Swahili
speaking countries and the African continent to showcase their talent, market
their creativity and network with clientele and the international fashion
industry.
This is all
aimed at emphasizing to the region that fashion is an income
generating creative industry, meanwhile promoting a "Made in Africa"
concept.
Swahili
Fashion Week is a platform founded and created by celebrated Tanzanian
couturier, Mustafa Hassanali in year 2008.
2013 marks the
Sixth edition of the Annual Swahili Fashion Week & Awards that will
be held in Dar-Es-Salaam from 5th - 8th December
2013.
CONTACT
PERSON: Kauthar Ally, Media & PR Manager
TELEPHONE
NUMBER: +255-718 855 590
EMAIL
ADDRESS: media@swahilifashionweek.com
SWAHILI FASHION WEEK YA SITA YAZINDULIWA
WABUNIFU 40 KUONESHA KAZI ZAO DAR ES SALAAM
JAMII YASISITIZWA KUUNGA MKONO UBUNIFU WA
NYUMBANI
Maonesho ya sita ya Swahili Fashion
Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar
Es Salaam, Tanzania.
Swahili Fashion week 2013 itakusanya
wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye
kwenda na wakati na kutegemewa kushika soko la Afrika Mashariki mwaka
2014.
“Swahili Fashion Week mwaka huu ina
lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni
zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka
ngazi za juu zaidi kila mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa
Swahili Fashion Week
Ukiwa ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya
wabunifu wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme)
“Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi yanayoashiria
mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa kitofauti na
mzuri.
“Tunasisitiza jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi
ya kikwetu, hasa kwa Tanzania. Vipaji vya nyumbani vinahitaji kukuzwa ili
kufikia majina yanayotambulika duniani katika tasnia hii. Hisani huanza
nyumbani, na ndio maana tunategemea kampuni pamoja na mashirika mbali mbali
kusaidia tasnia ya mitindo” Hamis K Omary, Meneja Masoko Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio,
Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa),
Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.
TAARIFA KWA WAHARIRI
KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion Week is ni jukwaa la wabunifu
wa mitindo na vito kutoka Nchi zinazozungumza
Kiswahili na Bara la Afrika kwa ujumla Kuonyesha ubunifu wao, kutafuta
masoko kwa ajili ya ubunifu na kujenga uhusiano na wateja pamoja na tasnia ya
mitindo kimataifa
Hii ni kwa nia ya kusisitiza kukua kwa
mitindo katika kanda ya
Afrika Mashariki na Kati na njia ya kipato ihusishayo tasnia ya ubunifu,
huku ikitangaza wazo la “Made in Africa”
Swahili Fashion Week imeanzishwa na
mbunifu mashuhuri Tanzania, Mustafa Hassanali mwaka 2008. Mpaka sasa ndio
maonyesho makubwa ya mitindo katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
2013 Itakua ni maonyesho ya sita ya
Swahili Fashion Week na Tuzo, ambayo yatafanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 5
– 8 Desemba 2013.
KWA
MAWASILIANO: Kauthar Ally, Media & PR Manager
SIMU:
+255-718 855 590
BARUA
PEPE: media@swahilifashionweek.com
--
SWAHILI FASHION WEEK
(East & Central Africas Largest Fashion Event)
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)784 303 880(SMS ONLY)
BB Pin: 2380CDB6
Networking : www.twitter.com/swahilifashion
www.facebook.com/
www.swahilifashionweek.
Web : www.swahilifashionweek.com