Sunday, July 28, 2013

Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) inaipeperusha vema Tanzania


Umoja wa Watanzania ujerumani(UTU) kwa kasi kubwa inaiwakilisha vema Tanzania huko Ughaibuni,kwa kutumia nafasi zote wanazopewa nchi Ujerumani, ni juzi kati tu Umoja huo ulishiriki katika maonyesho ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, ambapo wageni wengi walivutiwa sana na shughuli za Umoja huo za kuitangaza Tanzania, Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) unatilia mkazo sana katika kuwashawishi wadau wa kimataifa wawekeze katika udumua za jamii kama vile Elimu,Afya n.k. Umoja huo umepokea mialiko ya kushiriki maonyesho mengine yakiwemo makubwa kama International African Festival Tubingen 2013 yatakayo anza 8 hadi 11.08.2013 usikose kuwasiliana nao at kamati.utu@googlemail.com