Ngoma Africa Band Kutumbuiza mjini Bremen,Ujerumani Jumamosi 9.09.2017
FFU-Ughaibuni Kuzidi kuwatia kiwewe washabiki Ulaya !
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni yenye maskani nchini ujerumani,inatarajiwa kulitingisha jiji la Bremen siku ya jumamosi 9.09.2017 katika ukumbi wa Wisserterasse kuanzia saa mbili usiku,bendi hiyo iliyojijengea umaarufu katika kila kona kwa tabia zake za kuwadatisha akili washabiki wake katika majukwaa ya kimataifa kwa kutumia mdundo wake "Extraordinary Bongo Dansi" ndio bendi pekee ya kigeni barani ulaya inayodumu katika tasnia ya muziki kwa muda mrefu barani ulaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wa himaya yake ya viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com au wape hai at www.facebook.com/ngomaafricaband.
Comments
Post a Comment