Mamatembo blog: Jina la Mandozi limetoka wapi na linamaanisha
nini?
Armando Phili: Mandozi limetokana na jina langu Armando maana
yake shujaa. Hivyo Mandozi ni mashujaa kwa kilatino.
Mamatembo blog: Mandozi mnafanya michezo ya aina gani? Na mnachukua vijana wa kuanzia umri gani?
Armando Phili: Tuna michezo yote Iakini kwa sasa tumeanza na football (mpira wa miguu). Umri wa vijana wetu ni 16-19.
Mamatembo blog: Mmeanza lini? Nani mwanzilishi na kwanini
mmeamua kuanzisha Mandozi?
Armando Phili; Tumeanza 2013, tunamiaka 3. Armando Philly ndio mwanzilishi. Lengo letu ni kuwapatia vijana ajira, kuwaondoa katika makundi mabaya na kuiweka Tanzania katika ramani ya mpira.
Mamatembo blog: Mnafanyaje kupata
fedha za kukimu mahitaji ya kuendesha academy? Mnatoa vifaa au huduma gani kwa vijana
wanaojiunga na academy yenu (mfano hostel, chakula, jezi, viatu, n.k)?
Armando Phili: Mandozi Academy ni shule na vijana wataanza kuwa na hostel Kuanzia December. Mimi nilikuwa na pesa yangu million 45 niliwekeza hapo Mandozi Iakini bado ni mtaji mdogo sana. Ninaduka la matunda South uwa linanisaidia hivyo hivyo na vifaa. Sametime washikaji, kuna dada UK, jamaa Australia na jamaa Zanzibar
wananipa pesa elfu 50 kila mwezi.
Mamatembo blog: Ushawahi omba msaada serikalini kwenye Wizara husika? Au kwenye NGO's za
ndani na nje ya chini?
Armando Phili: Tumejaribu kutafuta lakini kimya au pia tunahitaji
connection za kutosha. kuna wadau wengine wana
connection hizo ila kukupa hawawezi.
Mamatembo blog: Mpaka sasa mna wanafunzi wangapi?
Armando Phili: Wapo 35.
Mamatembo blog: Wadau wanaweza kuwapata kwa njia gani?
Armando Phili; kwa simu ni 0785 46 44 61 na kwa website ya Mandozi Sports Academy www.mandozisportsacademy.org
·
Comments
Post a Comment