Katika harakati za kurekodi video za album ya Jipe Moyo yake muimbaji Felis Mwambalo Mubibya, muimbaji huyo ameamua kutoka kivingine na kutanguliza single kwa ajili ya wapenzi wa video hapa nyumbani, na kote duniani katika viwango vyakimataifa.
Single hii ambayo imerekodiwa na muimbaji Felis mwenyewe huko marekani, akimshirikisha muimbaji Mary Damian wa Strictly Gospel ambaye pia kwa sasa makazi yake yako hapo nchini marekani.
Muimbaji huyu ameamua kutowa wimbo huu baada ya kupokea maagizo toka juu, kama anavyosema, alisikia sauti ikimuambia, ni wakati wakutowa dhabiu ya shukrani kwa Mungu. Na kwakuwa Mungu wetu anatakiwa kupewa kilicho bora zaidi, basi aliamua kusimamisha kazi zingine nakutanguliza wimbo huu unaoitwa YEEHWO-Best friend (Rafiki mwema). Ukiangalia video hii utakubaliana nami kuwa Mungu wetu anastahili kilicho bora zaidi.
Katika kufanyikisha video hii, Felis alitoka Indiana anapoishi nakujiunga na Alex Joseck Jijini Cincinnati, Mji wa Ohio ambapo wimbo huu ulipofanyiwa shooting chini ya kampuni ya Kingdom Media iliyoko Ohio inchini Marekani, inayosimamiwa na bwana Alex Joseck.
Felis alikuwa na hili lakusema kuhusu kazi hii. " Nimeambiwa na Mungu niandae wimbo, na niutowe kama sadaka; kwa maana yakuutowa bure kwa kila mtu. kwahiyo nimetowa Yeehwo Best friend ambayo nimeitowa kwa free download. Yaani mtu yeyote anaruhusiwa kuunakili nakugawa na marafiki amendavyo" isipokuwa kuuza. Haki miliki bado iko kwangu.
Video hii inapatikana Youtube na kwenye TV station mbalimbali.
Pia kwa free donwload unaweza bonyeza link hizi:http://snd.sc/Qr8xKT
Wimbo huu unaeleza habari za huyu rafiki wakujivunia. Japo watu wote wanaweza kutuacha, yeye bado yuko nasi, bila kujalisha hali yetu ama tulivyo pinda.
Comments
Post a Comment