Wavuta bangi watatu baada ya kulivuta sana wakazima. Baada ya kushtuka wakamuona dogo anaangaika kuangua embe juu ya mti waliokuwa wameuegemea. Wakamfukuza dogo ili waangue wao. Jamaa waliangaika sana kurusha mawe juu bila mafanikio. Wakaendelea rusha mawe mengi lakini
hawakufanikiwa kuliangusha wala kuligusa. Mvuta bangi mmoja akasema;
"Isije ikawa tunahangaika hapa bureeee kumbe embe lenyewe bichi, ngoja nipande juu nikalicheki kwanza kama limeiva." Jamaa akapanda faster, baada ya dakika tano yule mvuta bangi akashuka chini na kuwaambia wenzake; "Ebwana daaah, kitu cha ukweli. Nimelibonyeza limeiva vizuri kabisaaa, tuendeleeni kuliangua tu wanangu." Jamaa wakaendelea kurusha mawe kutwa nzima
bila mafanikio!!!!
Author unknown
Comments
Post a Comment