Bondia wa Kike Mwafrika Bintou Yawa Schmill wa Ujeruamani



 Unapozungumzia mchezo wa ngumi au ndondi nchini ujerumani
Jina la Bondia wa kike mwafrika BINTOU YAWA SCHMILL A.K.A "THE VOICE"
ndiye anayemudu uringo "Boxing Ring" na kulipeperusha bara la
Afrika ughaibuni.


 Bondia  huyo kike  Bintou Yawa Schmill mwenye maskani kule
Drackenburg nje kidogo ya mji wa Bremen,amekuwa kivutio kwa
washabiki wa kimataifa na tishio kwa wapinzani wake anapokuwapo
ulingoni.


 Boxer Bintou Yawa Schmill mzaliwa wa Togo mwenye makao yake
nchini ujerumani alianza kucheza ngumi akiwa na umri mdogo
na kushinda mara 14 katika mashindan 24 na mara 4 K.O ,katoka
draw mara 2 uzito wa Water weight 63.5 Kg, katika ngumi za ridhaa.


  Kuanzia mwaka 2007 Boxer Bintou Yawa Schmill  a.k.a "The Voice"
alihamua kucheza kungumi za kulipwa kwa uzito wa Water weight 64.0 Kg,
mwenye urefu mita 1.70 amepigana na kushinda professional Record 4
 na Ushindi wa K.O mara 3.

Boxer Bintou Schmill kwa sasa kajiandaa kupambambana na bondia
yeyote yule wa kike na mahala popote  duniani.

http://www.bintou-schmill.de
You may book her at bongo4u@bongo-kwanza.com
http://www.youtube.com/watch?v=iEmjbWJrWxM

NYAMA CHOMA FESTIVAL


Umoja wa Watanzania Ujerumani kushiriki maonyesho ya Kimataifa mjini Aschaffenburg

 

Mhe.Mfundo,mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujerumani
 
Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya
"Brüderschaft der völker " mjini      Aschaffenburg " Ujerumani.
                   Kuanzia 19 hadi 21 Julai 2013

Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg,
nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayo
anza 19 hadi 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli
za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza
Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.
Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko
huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi
ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia
nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa
Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.
Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na

Official Trailer Remember Me Movie- by Oj's Production- India