Saturday, August 27, 2016

USITHUBUTU KUTIZAMA MPIRA UKIWA NA MWANAMKE NI QUESTION QUESTION STRESS TUPU

Mke: Honey timu gani zinacheza leo?

Mume: Arsenal vs Manchester Utd

Mke: oooh safi sana, ninaipenda Arsenal.

Mume: Safi hiyo timu nzuri sana, hujakosea Darling.

Mke: Drogba anacheza?

Mume: Drogba hachezei timu yoyote kati ya hizi zinazocheza hapa.

Mke: Okey sweety. Oh huyo ni Chriss Brown?

Mume: [akiwa ameboreka]
Hapana huyo ni Theo Walcott.

Mke: Ahaa ila wanafanana sana. Hiyo kadi ya njano aliyoonyeshwa huyo mchezaji n ya nin?

Mume: Hilo ni onyo kwa mchezaji aliyeonesha utovu wa nidhamu kwenye mchezo.

Baada ya dakika chache Wayne Rooney akafunga gori la kwanza kwa Manchester utd

Mke: [Huku akishangilia pasina kujua timu yake ndiyo iliyofungwa]
Oh oh Mume wangu Huyo ni walcot ndio amefunga goli ee?

Mume: [akiwa mpolee baada ya kufungwa]
Hapana sio Walcott ni Rooney ndio ameifunga Arsenal.

Mke: [akiwa amefura hasira]
Kwanini? Ilitakiwa Arsenal ndio ashinde.

Mume: [kimya]

Mke: Hiyo kadi nyekundu aliyoonyeshwa huyo mwenye kiduku ni ya nini?

Mume: [akiwa ameboreka kweli kweli]
Hiyo kadi nyekundu inamaanisha kwamba mchezaji atoke nje kutokana na kufanya madhambi uwanjani.

Mke: Kwaio akitoka nje anaenda kuwa kocha?

Mume: [akiwa amechoshwa na maswali ya mkewe huku akiwa hana utayari wa kujibu]
Aaaaaaaa Hapana wife. Anatoka nje kabisa hatakiwi kuonekana hata kwenye benchi la ufundi.

Mke: kwaio kadi nyekundu ni kama taa za barabarani.
Njano=Onyo
Nyekundu=Hatari

Mume: [akijibu tu ilimradi yaishe]
Haswaaa mke wangu, hivyo hivyo.

Mke: Vipi kuhusu kadi ya kijani

Mume: mmmmmh hapana kitu kama hicho katika mpira wa miguu.

Mke: Nataka Arsenal ishinde kombe la Dunia

Mume: [akaguna]
Kombe la dunia ni mashindano ya mpira wa miguu baina ya nchi na nchi na Arsenal sio nchi ni klabu ya mpira. Inacheza kwenye ligi ya Uingereza

Mke: Ni nani huyo mbaba aliyesimama amevaa koti refu na anapua ndefu anaefanana na Mr. Bean?b

Mume: [akiwa ameboreka haswa]
Huyo ni kocha wa Arsenal anaitwa Arsene Wenger.

Mke: Kwaio inamaanisha kwamba kocha wa hiyo timu pinzani anaitwa Machester Wenger?

Mume: [akabadilisha channel na kuweka TBC1 kipindi cha chereko
⚽🏃

No comments:

Post a Comment