Wednesday, September 9, 2015

Joke: Fomu toka kwa baba mkwe mtarajiwa.


FOMU YA MAOMBI YA KUMUOA BINTI YANGU

KIJANA, JAZA FOMU HII KWA MWANDIKO WAKO MWENYEWE NA KWA HERUFI KUBWA.

Mimi ......................., natuma ombi la kumuoa binti yako. Nina umri wa miaka ..............

TAFADHALI JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA UAMINIFU.

1. Huwa unahudhuria ibada? Ndiyo/Hapana
2. Una Masters au PhD? Ndiyo/Hapana
3. Una undugu au urafiki na tajiri yeyote mkubwa mjini? Ndiyo/Hapana
4. Mshahara wako una tarakimu 7? Ndiyo/Hapana
5. Unamiliki nyumba? Ndiyo/Hapana
6. Una gari? Ndiyo/Hapana

KAMA KATIKA MASWALI 6 HAPO JUU KUNA LOLOTE UMEJIBU HAPANA BASI USIENDELEE KUJAZA FOMU HII NA FUTA NDOTO ZA KUMUOA BINTI YANGU. KAMA MAJIBU YAKO YOTE NI NDIYO ENDELEA KUJAZA FOMU.

1. Kwa kutumia maneno yasiyopungua 50 elezea hasara za kuchepuka katika ndoa.

--------------------------------------
----------------------------------------------------------------------------------

2. Kwa kutumia mchoro elezea namna gani unaweza kuwapa heshima baba na mama mkwe wako.

3. Mfano mkeo akikwambia "Mume wangu nahitaji hela ya kwenda saluni" utamjibu vipi?

-----------------------------------------

4. Elezea sababu 10 za ndoa nyingi kuvunjika.

5. Elezea maana ya maneno "mume mwema" kama unavyoyafahamu wewe binafsi.

6. Wazazi wako wamefunga ndoa? Ndiyo/Hapana. Kama ndiyo, ndoa yao ina muda gani?

Kama umri wa ndoa ya wazazi wako ni mdogo kuliko umri wako elezea kwa nini ulizaliwa nje ya ndoa.

7. Elezea maana ya "Mume wangu urudi nyumbani mapema" kwa maneno yasiyopungua 100.

8. Toa sababu 3 ambazo zinaweza kumfanya mwanaume asilale nyumbani kwake na mkewe.

9. Ndoa ikivunjika, unadhani nani mmiliki wa watoto kati ya baba na mama.

JIBU MASWALI HAYA KWA KUANDIKA NDIYO AU HAPANA.

1. Unakunywa pombe?
2. Unavuta sigara?
3. Una hasira za karibu karibu?

HII NI SEHEMU YA MWISHO LAKINI MUHIMU KAMA NYINGINE ZOTE HAPO JUU

1. Lini uko tayari kuja kwangu kufanyiwa intaviu?

----------------------------------------

2. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji baba au mlezi wako wa kiume kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------
3. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji mama au mlezi wako wa kike kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------

4. Siku na muda gani unadhani ni sawa kumuhoji kiongozi wako wa kidini kuhusu hii nia yako?

-----------------------------------------

5. Tafadhali bandika picha yako ya rangi ya siku za karibuni ambayo itarushwa katika magazeti na mitandao ya kijamii ili kujua kama una wapenzi wengine.

Weka sahihi hapa:

-------------------------

Rudia kuweka sahihi hapa:

----------------------------------

Asante kwa kuonyesha nia ya kumuoa binti yangu. Muda wa kupitia maombi yako ni miezi 6. Utajulishwa kama tu utafanikiwa.

Niandikie anuani zako hapa chini ili niweze kukufikia kama nitakuwa na maswali zaidi.

E-mail: _________________
Simu: __________________
Facebook: ______________
WhatsApp: ______________
Twitter: _________________
Instagram: _______________
LinkedIn: _________________
BBM PIN: ________________

No comments:

Post a Comment