Thursday, April 7, 2016

Mandozi Sports Academy



Mamatembo blogJina la Mandozi limetoka wapi na linamaanisha nini?
Armando PhiliMandozi limetokana na jina langu Armando maana yake shujaa. Hivyo Mandozi ni mashujaa kwa kilatino.
Mamatembo blog: Mandozi mnafanya michezo ya aina gani? Na mnachukua vijana wa kuanzia umri gani?
Armando PhiliTuna michezo yote Iakini kwa sasa tumeanza na football (mpira wa miguu). Umri wa vijana wetu ni 16-19.
Mamatembo blog: Mmeanza lini? Nani mwanzilishi na kwanini mmeamua kuanzisha Mandozi?
Armando Phili; Tumeanza 2013, tunamiaka 3. Armando Philly ndio mwanzilishi. Lengo letu ni kuwapatia vijana ajira, kuwaondoa katika makundi mabaya na kuiweka Tanzania katika ramani ya mpira.
Mamatembo blogMnafanyaje kupata fedha za kukimu mahitaji ya kuendesha academy? Mnatoa vifaa au huduma gani kwa vijana wanaojiunga na academy yenu (mfano hostel, chakula, jezi, viatu, n.k)? 
Armando Phili: Mandozi Academy ni shule na vijana wataanza kuwa na hostel Kuanzia December. Mimi nilikuwa na pesa yangu million 45 niliwekeza hapo Mandozi Iakini bado ni mtaji mdogo sana. Ninaduka la matunda South uwa linanisaidia hivyo hivyo na vifaa. Sametime washikaji, kuna dada UK, jamaa Australia na jamaa Zanzibar wananipa pesa elfu 50 kila mwezi.
Mamatembo blogUshawahi omba msaada serikalini kwenye Wizara husika? Au kwenye NGO's za ndani na nje ya chini?
Armando PhiliTumejaribu kutafuta lakini kimya au pia tunahitaji connection za kutosha. kuna wadau wengine wana connection hizo ila kukupa hawawezi. 
Mamatembo blogMpaka sasa mna wanafunzi wangapi?
Armando PhiliWapo 35.
Mamatembo blogWadau wanaweza kuwapata kwa njia gani?
Armando Phili; kwa simu ni 0785 46 44 61 na kwa website ya Mandozi Sports Academy  www.mandozisportsacademy.org
·         


No comments:

Post a Comment